Pages

Ads 468x60px

Friday, November 15, 2013

KILIMANJARO STARS YAPANGWA KUNDI MMOJA NA MABINGWA WA ZAMANI WA AFRIKA KATIKA MICHUANO YA KOMBE LA CHALLANGE 2013.



Shirikisho la soka kwa nchi za ukanda wa Afrika ya mashariki na kati Cecafa limetangaza makudi ya timu zitakazoshiriki michuano ya Cecafa Challage Cup inayotaraji kuanza kuungruma nchini Kenya kuanzia Novemba 27  mwaka huu.

 Makundi hayo yamepangwa katika droo maalumu iliyofanyika  nchini Kenya ambapo wenyeji  Harambe Stars wametupwa katika kundi A  Tanzania bara “Kilimanjaro stars”ikiwa katika kundi  B  na kundi la tatu  yani kundi C linaongozwa na Uganda the Creans.

Katika michuano hiyo mchezo  wa ufunguzi  baina ya wenyeji Harambe stars na Ethiopia itachzwa kwenye uwanja  wa  Nyayo Stadium novemba 27.

Makundi ya michuano hiyo ni kama ifuatavyo hapa chini;-
Group A: Kenya, Ethiopia, Zanzibar, South Sudan
Group B: Tanzania, Zambia, Burundi, Somalia
Group C: Uganda, Rwanda, Sudan, Eritrea
Kwamujibu wa taarifa iliyotolewa na Cecafa  mzunguko wa kwanza  michezo itachezwa kwenye uwanja wa Nyayo michezo mingine itakuwa ikichezwa kwenye mji wa Machakosi .

Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment