Pages

Ads 468x60px

Friday, November 8, 2013



Timu ya soka ya Liverpool inayoshiriki ligi kuu ya England imetangaza nia ya kutaka kumtoa kwa mkopo mchezaji wake Rahim Sterling  mwezi januari mwakani lakini ni hadi wapate mchezaji mwenye uzoefu kuziba nafasi yake.

Kwamujibu wa chanzo kimoja cha habari barani Ulaya Liverpool imeanza mipango ya kumsajili nyota wa Sporting Lisbon ya Ureno Diego Capel na endapo wakiridhishwa nae watamchukua kama mbadala wa Sterling  ambaye ni raia wa England.
Mwanzoni mwa juma hili kocha wa Liverpool Brendan Rodgers alibainisha kwamba Sterling ni mchezaji ambaye anatakiwa kupambana  zaidi ili  aweze kuwa kwenye kikosi cha kwanza cha  majogoo hao wa Anfield.
Kwamsimu uliopita Rahim alionyesha uwezo mkubwa  baada ya kuichezea Liverpool michezo 36  na kisha kuitwa kwa mara ya kwanza kwenye timu ya taifa ya England.

Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment