Pages

Ads 468x60px

Monday, November 18, 2013

KIUNGO CESC FABRIGAS AANZA MAZOEZI MAPESI BAADA YA KUSUMBULIWA NA JERAHA LA GOTI.



Kiungo wa klabu ya soka ya Fc Barcelona Cesc Fabrigas ameanza mazoezi baada ya kuendelea kupona vyema jeraha lake la goti lililokuwa linamsumbua uongozi wa timu hiyo umethibitisha.
Mchezaji huyo jana mchana alianza mazoezi jana mchana na kushiriki  vipindi vyote  taarifa ya  klabu hiyo ambayo ni mabingwa wa ligi kuu ya Hispania imeeleza.
Aidha Barcelona kupitia tovuti yake imesema kuwa walinzi Gerard Pique na Jordi Alba wanaendelea na mazoezi ya pamoja na wenzao baada ya kuendelea vyema kutokana na  majeruha yaliyokuwa yakiwasumbua.
Fabrigas alimia goti la mguu wa kushoto kwenye mchezo ambao Barcelona ilishinda magoli 4 kwa 1 dhidi ya Real Betis mapema mwezi huu katika mchezo wa ligi kuu  jambo lililomfanya aondolewe kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Hispania.

Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment