Pages

Ads 468x60px

Monday, November 18, 2013

OZIL KUIKOSA ENGLAND KESHO,STURRIDGE NAYO KITENDAWILI.



Nyota wa timu ya taifa ya Ujerumani na klabu ya Arsenal Mesut Ozil ameondolewa kwenye kikosi cha kocha Joaquim Low kitakacho ikabili England hapo kesho kwenye mcchezo wa kirafiki wa kimataifa kwamujibu wa kaenda za fifa.
Ozil ameondolewa kwenye orodha ya weachezaji watakaocheza mchezo huo kutoakana na kusumbuliwa na jeraha ambalo alilipata katika mchezo baina ya Ujerumani na Italia uliochezwa ijumaa iliyopita na kutoka sare ya kufungana goli 1 kwa 1.
Kukosekana kwa Ozil ni pigo jingine kwa kocha wa Ujerumani baada ya kiungo Sami Khedira kuumia  goti kwenye mchezo uliopita wa kirafiki nakuelezwa kuwa atakaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita na anatarajiwa kufanyiwa upasuaji.
Katika mchezo na Italia Ozil aliingia  dakika ya 59 na nafasi kuchukua nafasi ya  Mario Gotze pambano ambalo Ujerumani ilitawala kwa kiwango kikubwa.
Katika hatua nyingine timu ya taifa ya England huenda ikamkosa mshambuliaji wake Daniel Sturridge kwenye mchezo huo baada ya hii leo kuondoka mazoezini kwakile kinachodhaniwa kuumia akiwa mazoezini.

 Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment