Tanzania imepanda kwenye msimamo wa ubora
wa soka duniani kwatakwimu zilizotolewa leo na shirikisho la soka duniani Fifa.
Takwimu hizo ambazo hutolewa kila
mwezi Tanzania ipanda kwa nafasi tano kutoka nafasi ya 129 mwezi uliopita hadi
katika nafasi ya 124 mwezi huu.
Katika takwimu hizo Uganda imeendelea
kushika nafasi ya kwanza kwa nchi
wanachama wa Cecafa kwakuwa nafasi ya 86 kidunia huku Ethiopia ikishika nafasi
ya pili kwa ukanda huo huku kidunia ikiwa nafasi ya 93.
Burundi ya 112 kidunia kwaukanda
Cecafa inashika nafasi ya tatu,Kenya ya 4 kwa ukanda huo ikiwa nafasi ya 117
kidunia huku nafasi ya 5 kwa ukanda wa Cecafa ikishikwa na Tanzania iliyopo
nafasi ya 124 kidunia.
Rwanda inashika nafasi ya 6 kwa
ukanda wa Cecafa ikiwa nafasi ya 127 kidunia,Sudani inashika nafasi ya 7 kwa Cecafa
huku ikishika nafasi ya 130 kwa dunia.
Katika msimamo huo wa ubora wa soka
duniani Eritrea inashika nafasi ya 8 kwa nchi wanachama wa Cecafa kidunia
ikishika nafasi ya 199,Sudan Kusini inashika nafasi ya 9 kwa ukanda wa Cecafa
wakati kidunia ikishika nafasi ya 201.
Somalia ndiyo inayoburuza mkia
kwenye takwimu hizo za obora wa soka duniani kwa nchi wanachama wa Cecafa
ikishika nafasi ya 10 huku kidunia ikishika nafasi ya 204.
mkule.blogspot.com
No comments:
Post a Comment