Pages

Ads 468x60px

Saturday, November 16, 2013

REAL MADRID YAPATA PIGO,KIUNGO SAMI KHEDIRA KUKAA NJE YA UWANJA KWA MIEZI SITA KUTOKANA NA JERAHA LA GOTI.



Kiungo wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ujeruman Sami Khedira atakuwa nje ya uwanja kwa miezi sita kutokana na kusumbuliwa na jeraha la goti.
Khedira mwezye umri wa mika 26 aliumia jana katika mchezo wa kirafiki baina ya timu yake ya taifa ya Ujerumani ilipokuwa ikicheza na Italia mjini Milan pambano liloloisha kwa sare ya kufungana goli 1 kwa 1.
Mchezaji huyo ambaye ameichezea timu ya taifa ya Ujerumani michezo 44 sasa anasubiri kufanyiwa upasuaji kutibu jeraha hilo
Akizungumza kwa masikitiko makubwa kocha wa Ujeruma Joachim Low  amesema anatambua mchango wa ntota huyo katika kikosi chake lakini anamatumaini  kwamba atapona kabla ya fainali zijazo za kombe la dunia zitakzofanyika mwakani nchini Brazil.
Kuumia kwa kiungo huyo si pigo kwa Ujerumani pekee bali hata kwa klabu yake ya Real Madrid ambayo inapigania ubingwa wa ligi kuu ya Hispania pamoja na kombe la klabu bingwa barani Ulaya msimu huu.

Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment