Kozi ya
wakufunzi wa mchezo wa riadha iliyokuwa ikifanyika katika chuo cha ualimu
Kleruu imemaliza leo kwakufungwa na katibu mkuu wa shirikisho la riadha nchini
RT Suleiman Nyambui huku wahitimu 31 wakikabidhiwa vyeti vyao.
Kozi hiyo
ambayo ilihusisha walimu mbalimbali wa shule za msingi wa chuoni hapo na walionje ya chuo hicho
ilikuwa ikihusisha mafunzo ya daraja la kwanza na la pili ambapo jumla ya
wahitimu waliomaliza ni 31.
Kati ya hao
waliohitimu daraja la kwanza ni 12
wanawake watano wanaume 7 huku daraja la pili wakihitimu watahiniwa
19 wanawake 8 wanaume 11.
Akizungumza
katika hafla maalumu ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu hao katibu mkuu wa
Shirikisho la riadha nchini RT Suleiman Nyambui amewataka wahitimu kutumia
vyema mafunzo waliyoyapata katika kuendeleza mchezo huo.
Nyambui
amesema jitihada kubwa zinahitajika kurejesha heshima ya mchezo wa riadha
iliyopotea kwa muda mrefu huku akitoa
rai kwa vyuo mbalimbali kutoa mafunzo ya riadha kwa wanafunzi kwa lengo la kuuendeza
mchezo huo.
Amesema wao
kama shirikisho wapo tayari kufika mahala popote kutoa mafunzo za ukufunzi wa
mchezo wa riadha bila malipo yeyote kikubwa ni kugharamia nauli za wakufunzi
chakula pamoja na malazi kwa muda ambao kozi itakuwa ikitolewa.
Aidha
ameushukuru uongozi wa chuo cha ualimu Kleruu kwa kuwa mstari wa mbele
kuendeleza riadha kwatoa fursa kwa walimu chuoni hapo kupata mafunzo hayo.
Naye mgeni
rasmi katika hafla hiyo afisa michezo mkoa wa Iringa Kenethi Komba ameseahidi
kushirikiana na chuo cha Kleruu pamoja na shirikisho la riadha nchini RT katika harakati za kuendeleza mchezo huo
mashuleni.
Amesema
kushuka kwa mchezo wa riadha nchini kunatokana na serikali kuondoa michezo
mashuleni kabla ya kuirejesha tena huku akiwaomba wahitimu kutumia vyema
mafunzo waliyoyapata kwenye maeneo yao
ya kazi.
Kozi hiyo
ilikuwa ikisimamiwa na mkufunzi mkuu anayetambuliwa na shirikisho la riadha
nchini RT ndg.Samweli Tupa ambaye
alikuwa kivutio kikubwa kwa wahitimu hao kutokana na ucheshi alionao katika ufundishaji.
Mgeni
rasmi akitoa cheti kwa mmoja wa wahitimu wa kozi hiyo mchana wa leo.
Katibu
mkuu wa rt Suleiman Nyambui akizungumza na wahitimu wa kozi hiyo katika chuo
cha kleruu katikati ni mgeni rasmi Keneth Komba ambaye ni afisa michezo mkoa wa
iringa na wapembeni yake ni mwl.Samweli Tupa aliyekuwa mkufunzi wa kozi hiyo.
Wahitimu
katika igizo la huwezi kumtambua mwathika wa ugonjwa wa ukimwi kwa kumwangalia
ambapo kila upande mtu mmoja alipatiwa kitu wakiwa wamefumba macho na kisha
kuanza zoezi la kukisia ni nani anaedhaniwa kuwa mwathirika kwakuangalia
mshindi ni aliyepatia mtu mwenye kitu alichopewa na mmoja wa washiriki.
Mkufunzi Samweli Tupa akizungumza jambo mbele ya wahimu hao mchana wa leo .
Posted by Yusuph Mkule.
No comments:
Post a Comment