Pages

Ads 468x60px

Thursday, November 21, 2013

MOHAMED ZIDAN AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 6 JELA.



Zidan akiwa  katika jezi ya timu ya taifa ya Misri.

Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Misri na Klabu vya Borussia Dortmund amehukumiwa kwenda jela miaka 6 baada ya kukutwa na kosa la kuandika cheki tatu za uongo kwenye kampuni  mmoja ya kibiashara iliyopo Misri.
Kwamujibu wa vyombo vya habari nchini Misri mahakama imemkuta na hatia mchezaji huyo  na kujiridhisha mtuhumiwa kutenda kosa hilo kwenye kampuni hiyo hivyo atatumikia kifungo hicho .
Zidan mwenye umri wa miaka 31 enzi za uchezaji wake alifanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Ujerumani Bundesiliga alkiwa na Borussia Dortmund huku akishinda ubingwa wa Afrika mara mbili akiwa na timu ya taifa ya Misri.
Hadi anakutwa na mkasa huo wa kuhukumiwa kwenda jela miaka sita Zidan alikuwa akifanya kazi katika shirika la habari la Aljazira mjini Doha kama mchambuzi wa michezo kwenye kituo hicho.

Hapa Zidan akiwa na uzi wa timu ya taifa ya Misri kwenye mchezo dhidi ya Brazil 
 

Hapa akiwa na jezi ya klabu ya Borussia Dortmund ya nchini Ujeruman. 

Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment