Pages

Ads 468x60px

Friday, November 8, 2013

SIMBA SPORTS CLUB.




Wakiwa na vijana Wengi kwakiasi chao wameonyesha uwezo ambao si mbaya sana wala sio mzuri sana.
Kibadeni na benchi lake la ufundi wamejaribu kuisuka timu yenye vijana wengi diyo,wamejaribu kutuonyesha kwanini walipanga kuileta Simba yenye sura mpya lakini bado pengo la Kaseja limeonekana wazi huku Abeli Dhaira akioneka akishindwa kuhimili kashikashi.
Sikushangaa kuona akifungwa magoli yakizembe licha ya safu ya ulinzi kujaribu kumfichia udhaifu wake akiwa katika milingoti mitatu hali ambayo ilimfanya kocha mkuu Abdaah King Kibaden kuonyesha hofu yake kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya wageni wa ligi Ryhno Rangers ya Tabora.
Ushauri wangu kwa simba wasimfukuze kocha na benchi lake la ufundi kwakupata matokeo yasioridhisha kwenye duru ya kwanza chamsingi wampe nafasi Kibadeni kuijenga timu hiyo kwa kutumia uzoefu wake na taaluma yake ya ukocha.
Angalizo,Kamwe asingiliwe na yeyote kwenye kazi yake,msemaji afanye kazi yake,katibu afanye kazi yake,mwenyekiti naye afanye kazi yake kwakuzingatia katiba ya Simba.
Ni hayo tuu Jamani…………………….

Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment