Pages

Ads 468x60px

Friday, November 8, 2013

YANGA AFRIKA.



Mabingwa wa ligi kuu ya soka Tanzania bara timu ya Yanga  wamefanikiwa kumaliza duru ya kwanza  msimu huu wa 2013/2014 wakiongoza  ligi baada ya kufanikiwa kuinyuka Jkt Oljoro ya mkoani Arusha  magoli  3 kwa 0 pambano lilochezwa  hapo jana kwenye dimba na taifa jijini Daresalaam.

Yanga ambayo ilianza ligi kwa kusuasua   imefanikiwa kuvuna alama 28 katika michezo 13 waliyocheza msimu huu wakishinda michezo minane,kwenda sare minne na  kufungwa mchezo mmoja pekee chini ya kocha mkuu Arne Brandts   raia wa Uholanzi.

Kwaufupi Yanga wameonyesha  uwezo mzuri  licha ya kukabiliwa na upinzani mkubwa kwenye michezo yao ya ugenini msimu huu lakini wameendelea  kuwa wakomavu kwa kuutumia vyema uwanja wao wa nyumbani wa taifa kila wanapocheza.
Je,kasi waliyomaliza nayo wataanza nayo vijana hao  wenye kibarua cha kuutetea ubingwa mbele ya Mbeya City na Azam walioonyesha upinzani mkubwa msimu huu?

Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment