Pages

Ads 468x60px

Friday, November 22, 2013

VIDIC KURUDI UWANJANI MWISHONI MWA JUMA HILI.





Kocha mkuu wa mabingwa wa ligi kuu ya England Manchester United David Moyes amethibitisha kuwa mlinzi  Nemanja Vidic atarejea uwanjani mwishoni mwa juma hili ambapo Man U itakuwa ugenini kucheza na Cardiff City.
Matumaini ya kumrejesha uwanjani Vidic yanatokana na kuendelea vyema kutokana na jeraha aliloumia kwenye pambano dhidi ya Arsenal ambapo Arsenal ililala kwa kufungwa goli 1 kwa 0 lililofungwa na Rubin Vab Persie.
Kocha David Moyes amesema jeraha alilokuwanalo Vidic lilimlazimu apumzike kwa muda mrefu hivyo anaamini nyota huyo raia wa Serbia ameshapumzika vyakutosha na ni wakati wake wa kurudi uwanjai kuitumikia timu yake.
Wakati Vidic akirejea uwanujani juma hili matumaini mengine ya United yapo kwa kiungo Michael Carrick ambaye naye anaendelea vyema kupona na anatarajiwa kurudi dimbani siku chache zijazo.
Wakati huohuo klabu ya Manchester United leo imerefusha  mkataba wa  kiungo Michael Carrick mwenye umri wa miaka 32 utakaomfanya aendelee kuwepo Old Traford hadi  mwezi juni mwaka 2015.
United pia itamkosa Danny Welbeck amabye anataraji kufanyiwa upasuaji wa goti linalomsumbua lakini pia United kwenye mchezo wa keshokutwa  huenda ikamkosa Phil Jones ambaye aliumia akiwa akiitumiakia na timu ya taifa.

Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment