Pages

Ads 468x60px

Friday, November 8, 2013



Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Wales Chris Coleman  leo anataraji kukutana na uongozi wa shirikisho la soka nchini humo kufanya mazungumzo ya kupewa mkataba mpya wa kuendelea kuifundisha timu hiyo.
Coleman mwenye umri wa miaka 43 ambaye mkataba wake wasasa unamalizika  baada ya mchezo wa kirafiki baina ya Wales na Finland tarehe 16 ya mwezi huu  pia anahusishwa na mipango ya kujiunga na timu ya Crystala Palace ya England.
Coleman ambaye alianza kuifundisha Wales mwezi januari mwaka jana  kuchukua nafasi ya Gary Speed aliyefariki dunia  mara baada ya mazungumzo ya leo na uongoizi wa shirikisho la soka nchini humo anatarajiwa kutangana kikosi cha timu ya taifa.
Akiwa kocha wa Wales Coleman amekiongoza kikosi chake katika michezo 15 akishinda minne,kwenda sare miwili na kufungwa michezo tisa huku akishindwa kuivusha nchi hiyo kwenye fainali zijazo za kombe la dunia mwakani huko Brazil.

Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment