Bodi ya wadhamini wa klabu ya Simba imesema haitambui
maamuzi yaliyotolewa na kamati ya Utendaji ya klabu hiyo kuhusiana na
kumsimamisha mwenyekiti Ismail Aden Rage pamoja na benchi la ufundi.
Mwenyekiti wa baraza la wadhamini Hamisi
Kilomoni amesema kuwa wao kama bodi wamesikitishwa na hatua hiyo ya kamti ya Utendaji nakuongeza kuwa hawana barua juu ya mabadiliko hayo ya kumsimamisha rage.
Kilomini amsema wao hawaungi mkono migogoro na kwamba wanachopenda nikuona Simba ikiwa na maendleo mazuri kwakuwa na uongozi wenye mshikamano wa dhati.
Amesema nia ya bodi hiyo ni kuijenga Simba na kuwakosoa wale wote wanaofanya maamuzi ya kukurupuka juu ya mambo mbalimbali ya klabuni mwao.
Kilomo hakusita kutangaza nia na msimamo wa bodi hiyo hiyo ya
udhamini katika kuijenga Simba ambayo imeshindwa kuonyesha cheche zake katika
duru ya kwanza ya ligi kuu Tanzania bara.
Posted by Yusup Mkule.
No comments:
Post a Comment