Timu ya taifa ya Cameroon imefanikiwa kufuzu fainali zijazo za kombe la dunia baada ya kuifunga Tunisia jioni ya leo magoli 4 kwa 1.
Ikicheza kwenye aridhi ya nyumbani Cameroon imepata magoli yake kupitia kwa Pierre Webo dakika ya 4 huku ya magoli mengine yakifungwa na Benjamin Moukandjo Bilé na Jean Makoun aliyefunga magoli mawili huku goli la kufutia machozi kwa Tunisia likifungwa na Ahmed Akaïchi.
Cameroon iliyokuwa ikiongozwa na nahodha wake Samweli Eto'o ilicheza mchezo wa kasi na nguvu nyingi jambo lililowawia vigumu wapinzani wao kufurukuta.
Katika mchezo wa awali mataifa hayo yalitoka suluhu ya bila kufungana pambano ambalo Tunisia ilikuwa mwenyeji. Keshokutwa kutakuwa michezo mingine ya kufuzu kwa kombe la dunia barani Afrika itachezwa siku ya jumanne ambapo Misri itaikaribisha Ghana huku Mbweha wa jangwani Algeria watakuwa wenyeji wa Burkinafaso.
Posted by Yusuph Mkule.
No comments:
Post a Comment