Pages

Ads 468x60px

Saturday, November 9, 2013

MANCHESTER UNITED KUMKOSA DANNY WELBECK KESHO DHIDI YA ARSENAL KATIKA MFULULIZO WA LIGI KUU YA NCHINI ENGLAND.




Kuelekea katika mchezo wa kesho kati ya Manchester United na Arsenal uongozi wa klabu ya Manchester umesema mshambuliaji Danny Welbeck ataukosa mchezo huo kutokana na kupatwa na jeraha la goti.

Nyota huyo wa kimataifa  wa  England aliumia goti katika mchezo dhidi ya Fulham uliochezwa hivi karibuni na United kushinda magoli 3 kwa 1 .Pia jeraha hilo lilimfanya akose  mchezo wa klabu bingwa Ulaya dhidi ya Real Sociedad  mwanzoni mwa juma hili.

Kocha wa Manchester United, David Moyes amesema hilo ni pigo kwa klabu lakini  anataraji kumtumia Robin Van Persi, Wayne na Javier Hernandez “Chicahrito” katika safu ya ushambuliaji.

Manchester United inayoshika nafasi ya 8 katika msimamo wa ligi kuu nchini England inataraji kuwakaribisha vinara wa  BPL klabu ya Arsenal pambano linalotaraji kuchezwa  majira ya saa 1 na dakika 10 usiku kwa saa za AfrikaMashariki hapo kesho.

Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment