Timu ya
taifa ya Tanzania bara Kilimanjaro stars leo imetoka sare ya kufungana goli 1
kwa 1 na timu ya taifa ya Zambia Chipolopolo kwenye mashindano ya kombe la Challenge
yaliyoanza jana nchini Kenya.
Katika
pambano hilo Zambia ndiyo iliyokuwa yakwanza kupata goli kupitia kwa mchezaji Ronald
Kampamba Dkk ya 41 Kabla ya Kili stars kusawazisha kunako dkk ya
48 likifungwa kwa kichwa na Said Morad.
Baada ya
mchezo kumalizika kocha mkuu wa Kilimanjaro Stars Kim Poulsen amesema
ameridhika na uwezo wa kikosi chake hivyo anamatumaini ya kufanya vyema michezo
inayofuata.
Kim pia
amesema wachezaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaoichezea TP Mazembe ya
DRC Congo watakuwepo katika michezo inayofuata baada yah ii leo kukosekana kwenye
kikosi hicho.
Naye
kocha mkuu wa Chipolopolo mfaransa Patrice Beaumelle amezipongeza timu zote
kwakucheza soka safi huku akieleza
matarajio yake kwenye michezo inayofuata kwakusema matokeo waliyoyapata ni
mwanzo mzuri hivyo hanashaka yeyote na michezo inayofuata.
Kwaupande
wake kiungo Salum Aboubakary wa Kili stars ambaye alichaguliwa nyota wa mchezo
amesema kikosi chao kimecheza vibaya ungwe ya kwanza lakini kipindi cha pili
walibadilika na hatimae kusawazisha goli na hatimae kupata sare hiyo.
Pia
kiungo huyo ambaye ni mtoto wa nyota wa zamani wa klabu ya Yanga na timu ya taifa
ya Tanzania Aboubakari Salumu “sure boy amelalamikia uwanja wa Kenyatta uliopo Machakosi walioutumia leo
kuwa haukua mzuri hasa baada ya mvua kunyesha.
Kwa
matokeo hayo, Burundi inaongoza kundi hilo baada ya kuifunga Somalia 2-0 katika
mchezo wa kwanza wa kundi hilo.
Kikosi
cha Stars kilikuwa; Ivo Mapunda, Himid Mao, Erasto Nyoni, Said Morad, Kevin
Yondan, Frank Domayo, Salum Abubakar ‘Sure Boy’/Ramadhani Singano ‘Messi’ dk89,
Hassan Dilunga/Athumani Iddi ‘Chuji’ dk85, Elias Maguri/Haroun Chanongo dk72,
Amri Kiemba na Mrisho Ngassa.
Chipolopolo;
Nsabata Toaster, Bronson Chama, Jimmy Chisenga/Kabaso Chongo dk67, Christopher
Munthali, Rodrcik Kabwe, Stanley Nshimbi/Alex Nshimbi dk57, Sydney Kalume,
Kondwani Mtonga, Felix Katongo/Salulani Phiri dk73, Ronald Kampamba na Festus
Ndewe.
Kwenye mchezo
wa awali hii leo Burundi ilifanikiwa kuifunga Somalia magoli 2 kwa 0
Kesho ni
zamu ya Sudan na Eritrea kwenye uwanja wa Kenyata uliopo Machakosi majira ya
saa nane kamili mchana wakati mabingwa watetezi Uganda wataikabili Rwanda
kwenye uwanja huohuo wa Kenyatta saa kumi jioni.
mkule.blogspot.com
No comments:
Post a Comment