Pages

Ads 468x60px

Wednesday, November 13, 2013

ENGLAND YAENDELEA KUTABIRIWA MABAYA FAINALI ZA MWAKANI ZA KOMBE LA DUNIA.



Pamoja na kupata tiketi ya kucheza fainali za kombe la dunia mwakani  England imeendelea  kutambiriwa kutofanya vyema kwenye michuano hiyo  itakayofanyika nchini Brazil kwakushirikisha mataifa mbalimbali.
Kauli iliyotolewa na mchezaji wa zamani wa Manchester United Owen Hargreaves  imemkariri raia huyo wa England akisema ni vigumu kwa nchi hiyo kutwaa ubingwa wa dunia mwakani kutokuwa na kubadilika kila mara.
Pamoja na kuwa na wachezaji wazuri Hargreaves bado  haipi nafasi England  kushinda kombe hilo ambalo imelitwaaa mara mmoja katika ardhi ya nyumbani mwaka 1966 licha ya kukisifia wachezaji wenye uwezo  kwenye timu hiyo.
Tangu itolewe kwenye michuano ya kombe la mataifa ya Ulaya mwaka 2012 England inayofundishwa na kocha Roy Hodgson  imepoteza mchezo mmoja kati ya 16 iliyocheza.

Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment