Timu ya
taifa ya Uruguay imefanikiwa kuingia katika michuano ya kombe la dunia huko
nchini Brazil mwaka 2014 baada ya kutoa suluhu na timu ya taifa Jordan.
Taifa hilo
kutoka bara la Amerika ya kusini limekuwa ndio timu ya mwisho kufanikiwa
kuingia katika mashindano hayo na kukamilisha idadi ya timu 32 kutoka mabara
matano tofauti.
Katika
mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Jordan, Uruguay iliibuka na ushindi wa
magoli matano kwa sifuri hivyo imepita kwa idadi hiyo ya magoli.
Uruguay
ambao ni ni mabingwa wa dunia mara mbili inashika nafasi ya 6 katika orodha ya
ubora wa shirikisho la soka duniani (FIFA) walifika hatua ya nusu fainali katika
kombe la dunia mwaka 2010 lililofanyika nchini Afrika ya kusini.
Posted by Yusuph Mkule.
Golikipa wa timu ya taifa ya
Hispania na klabu ya FC Barcelona Victor Valdes amepata jeraha la msuli
litakalomuweka nje ya uwanja kwa mudawa mwezi mmoja na wiki mbili.
Valdes amepata jeraha hilo katika
mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Afrika ya kusini ikiwa ni dakika
25 baada ya kuchukua nafasi ya Iker Cassilas.
Mhispania huyo ameshacheza michezo
19 msimu huu katika klabu ya Barcelona na ameshatangaza kuwa anataraji kuihama
klabu hio mwishoni mwa msimu wa mwaka 2013/2014.
Valdes anataraji kukosa michezo
miwili ya klabu bingwa Ulaya na miwili ya ligi kuu nchini Hispania (La Liga)
huku akitizamiwa kurudi mwezi wa kwanza mwaka 2014.
Posted by Yusuph Mkule.
Mlinzi
wa timu ya Liverpool kufanyiwa upasuaji wa goti linalomsumbua………………
Kocha
mkuu wa klabu ya Liverpool Brendan Rodgers amethibitisha kuwa mlinzi wa timu hiyo Jose Enrique anahitajika
kufanyiwa upasuaji wa goti kutokana na
jeraha alilonalo.
Rodgers ambaye kikosi chake kimeanza vyema msimu huu
wa ligi amebainisha kwamba raia huyo wa
Hispania anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na upasuaji
atakaofanyiwa.
Mchezaji
huyo ambaye aliumia kwenye pambano la timu yake ya Liverpool na Manchester United
mwezi wa tisa mwaka huu alirejea uwanjani mwanzoni mwa mwezi huu na kucheza
pambano dhidi ya Fulham ambapo Liver ilishinda magoli 4 kwa 0.
Kwasasa
kikosi cha Liverpool kinashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kikiwa na
alama 23 nyuma ya Arsenal ambayo inaoongoza kwa alama 25.
Posted by Yusuph Mkule.
Timu ya soka ya AS Roama ya Italia
imeingia kwenye kinyang’anyiro cha
kutaka kumsajili nyota wa Fc Lille ya
Urafansa Solomon Kalou ambae pia anawaniwa na vinara wa ligi kuu ya England
Arsenal.
Kwamujibu wa gazeti mmoja barani Ulaya kocha Rudi Garcia amenukuliwa akisema yupo
kwenye mipango ya kuimarisha kikosi chake cha
Roma kwenye msimu wa usajili mwezi januari mwakani baada ya kuanza vyema
msimu huu wa ligi ya Italia.
Roama ambayo haijafungwa michezo 12
ya ligi msimu huu na kushinda mipambano 10
wanauwezekano wa kumsajili raia huyo wa Ivory Coast ambaye alijiunga na Lille akitokea Chelsea ya
England kutokana na uwezo alionao.
Kalou ambaye anaumri wa miaka 28
hivi karibuni amefunga goli la 23 katika timu ya taifa kwenye mchezo dhidi ya
Senegal uliomalizika kwa sare ya goli 1 kwa 1na hatimae kufuzu fainali za kombe
la dunia zitakazofanyika nchini Brazil mwakani.
Posted by Yusuph Mkule.
No comments:
Post a Comment