Kocha wa klabu ya Arsenal raia wa Ufaransa Arsene Wenger anaamini kuwa kikosi chake alichokijenga kwa vijana wengi kitaiadhibu Manchester United hii leo kwenye mchezo wa ligi kuu ya England unaotaraji kuchezwa milango ya saa 1 na dakaka kumi usiku wa leo Old Traford.
Mfaransa huyo anayejifunia mwenendo mzuri
walioanza nao msimu huu kwenye ligi kiasi cha kushikilia usukani hadi sasa
anakifananisha kikosi chake na kile cha Man United cha mwaka 1992 kilichotwaa ubingwa wa tano wa ligi kuu ya
England.
Wenger amewataja wachezaji wa Manchester
United mwaka huo wa 1992 kama Ryan
Giggs,Paul Schole,Nick Butt,David Bekham
kwamba ni kati ya kikosi anachoamini kilikuwa bora sana kwa United kama
Arsenal ya sasa aliyoijenga kwa muda mrefu.
Wenger ametaja wachezaji wake vijana
anaoamini kwa umri wao hakuna wa kuwazuia kufanya vyema simu huu hatimae kutwaa
ubingwa.
Amewataja wachezaji Aaron Ramsey, miaka 22, Jack Wilshere, 21,
Theo Walcott, 24, Alex Oxlade-Chamberlain, 20, Kieran Gibbs, 24, na Wojciech
Szczesny miaka 23 kwamba kwa uwiano wa umri wao wanauwezo wa kuisaidia Arsenal
kwa kiasi kikubwa.
Wenger anajifunia safu nzuri ya ushambuliaji aliyonayo
ikiongozwa na Aaron Ramsey aliyefunga magoli 11 msimu huu likiwemo goli
alilowafunga Borussia Dortmund kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya juma hili.
Arsenal inaikabili Man United kwenye uwanja
wa Old Traford ikiwa inaongoza ligi kwa
alama 25 huku United ikiwa na alama 17
ikiwa ni tofauti ya alama 8 timu zote zikiwa zimecheza michezo 10 pekee.
No comments:
Post a Comment