Pages

Ads 468x60px

Wednesday, November 27, 2013

UPASUAJI WA AYEW WAENDA SALAMA SASA KUKAA NJE YA DIMBA KWA MIEZI MIWILI.





Klabu ya soka ya Marseille ya Ufaransa imetangaza kuwa nyota wake raia wa Ghana Andre Ayew  amefanyiwa upasuaji wa goti lake lililokuwa linamsumbua na upasuaji huo umeenda salama.

Ayew ambaye  aliitumikia Ghana kwenye mchezo wa play off kufuzu kombe la dunia wiki iliyopita dhidi ya Misri upasuaji  wake umefanyika jana chini ya daktari Jean-Piere Francesnch na anatarajiwa kutoka hospitalini kesho.

Taarifa hiyo imearifu kuwa raia huyo wa Ghana anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi 2 na anatarajiwa kurejea uwanjani mwezi January mwakani.

Ayew  akiwa na kikosi cha Marseille msimu huu wa ligue one  amefunga magoli 8 katika michezo 9 aliyocheza huku akiwa amecheza kwa kusuasua kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti.

mkule.blogspot.com

No comments:

Post a Comment