Mwenyekiti wa klabu ya Simba Ismail
Aden amesema kuwa yupo tayari kujiuzuru nyazifa yake kuliko kuitisha
mkutano wa wanachama siku kumi na nne zilizotolewa na Uongozi wa Shirikisho la
soka nchini TFF.
Rage amekaidi amri hiyo leo
baada ya uongozi wa Shirikisho la soka nchini TFF kupitia kwa Rais wake Jamal Malinzi kuwa aitishe mkutano ndani ya siku 14 kuanzia jana.
Amesema hayupo tayari kuvunja katiba
ya Tff na ya Simba kwashinikizo la watu wachache wanaotumiwa kuivuruga Simba
tena mbaya zaidi anapangiwa muda na ajenda za mkutano huo kitu ambacho hakipo
kwenye katiba ya Simba na ya TFF.
Rage amesema hataitisha mkutano
wowote ndani ya Simba na ataendelea na
madaraka yake kama kawaida ya kuiongoza klabu hiyo.
Aidha Rage ameiomba TFF
iheshimu katiba ya Simba ili uongozi wa timu hiyo ufanye kazi ya kutekeleza
majukumu yao.
Wakati huohuo, Mwenyekiti wa Simba
Ismail Aden ameteuwa Michael Wambura kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji, huku
Rahma Alharoos malkia wa nyuki wamemuomba awe mdhamini wa klabu
hiyo.
Hata hivyo amesema tuhuma
anazopewa kuhusu kula pesa za mchezaji
wake wa zamani Emanuel Okwi sio za
kweli kwakuwa usajili huo hakutangazia chumbani na mke wake aliutangazia umma
wa Tanzania na kila mtu alisikia.
Posted by Yusuph Mkule.
No comments:
Post a Comment