Pages

Ads 468x60px

Saturday, November 16, 2013

WOJCIECH SZCZESNY AREFUSHA MKATABA WAKE NA VINARA WA BPL TIMU YA ARSENAL.



Mlinda mlango wa vinara wa ligi kuu ya nchini England Arsenal  Wojciech Szczesny amesaini mkaba mpya utakaomfanya aendelee kuvaa uzi wa The Gunners  kwa kipindi kirefu zaidi.
Raia huyo wa Poland mwenye umri wa miaka 23 tangu ajiunge na Arsenal akitokea Legia Warsaw mwaka  2006 ameichezea Arsenal michezo 123  huku akidakia timu ya taifa lake kwa mara ya kwanza mwezi September mwaka 2009.
Szczesny ambaye ni mtoto wa golikipa wa  zamani wa timu ya taifa ya Poland Maciej Szczesny hata hivyo mkataba wake huo haujawekwa wazi utaisha lini lakini kocha wa Arsenal amemzungumzia  nyota huyo kuwa anakipaji kikubwa ndiomaana wamerefusha mkataba wake.
Mchezaji huyo ambaye amekuwa Tengemeo kwa Arsenal inayoongoza ligi kwa alama  25 msimu huu hadi sasa amesema anajivunia kuwa mchezaji wa Arsenal na anandoto kubwa ya kupatia mafanikio timu hiyo.
Mchezaji huyo aliichezea Poland mchezo wa 15  mwezi oktoba mwaka huu  kwenye uwanja wa Wembley ambapo ilikuwa ikicheza na England kutafuta tiketi ya kucheza kombe la dunia mwakani.

Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment