Pages

Ads 468x60px

Tuesday, November 19, 2013

VITA NYINGINE YA KUGOMBEA TIKETI YA KUFUZU FAINALI ZIJAZO ZA KOMBE LA DUNIA KWA MATAIFA YA AFRIKA KUFANYIKA LEO.

Ni kivumbi na jasho hii leo nchini Misri ambapo timu ya soka ya taifa hilo maarufu kama Mafarao itakapoikaribisha  Ghana kwenye mchezo wa marudiano kufuzu kwa fainali zijazo za kombe la dunia zitakazofanyika mwakani nchini Brazil.

Ghana ambayo ilishinda katika mchezo wa awali kwajumla ya magoli 6 kwa 1 imejawa na hofu kubwa kutokana na hali ya kiusalama ilivyo kwenye taifa hilo la kaskazini mwa bara la Afrika kiasi cha kutuma ujumbe maalumu juma lililopita kwenga nchini Misri kuthibitishiwa usalama wa wachezaj na mashabiki wao hii leo.

Pamoja na hilo kama hiyo haikutosha waziri wa michezo nchini Ghana mwezi uliopita aliandika barua kwa rais wa Fifa Sepp Blatter akimtaka awathibitishie kuwa raia wa Ghana  na wachezaji wa timu yao ya taifa watakuwa kwenye ulinzi wakutosha kutokana na hali tete ilivyo kwenye taifa la Misri.

                     Hiki ni kikosi cha timu ya taifa ya MISRI maarufu kama mafaraooo

 
                               Hiki ni kikosi cha timu ya taifa ya Ghana...BLACK STARS.


Kwaupande mwengine timu ya taifa ya Algeria itakuwa nyumbani kuikaribisha Burkinafaso kwenye mchezo mwengine wa marejeano kufuzu kombe la dunia pambano ambalo Burkinafaso itaingia ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa magoli 3 kwa 2 kwenye mchezo wa awali.

h
Hiki ni kikosi cha timu ya taifa ya Algeria maarufu kama Mbweha wa jangwani.

h
                            Hiki ni Kikosi cha timu ya taifa ya Burkinafaso maarufu kama Farasi.

No comments:

Post a Comment