Pages

Ads 468x60px

Monday, November 18, 2013

SCOLARI BADO AITAMANI CHELSEA.



Kocha wa timu ya taifa ya Brazil Luiz Felipe Scolari amesema kuwa anapenda kufundisha soka nchini England licha ya kuudhiwa alipokuwa anaifundisha Chelsea mwaka 2008.
Scolari ambaye alidumu kwa muda wa miezi saba alipokuwa kocha wa Chelsea amesema alipenda kuifundisha timu hiyo kwa misimu miwili au zaidi  kutokana na alivyokuwa akiijenga timu hiyo lakini alisikitishwa na uamuzi wa kufukuzwa na mmiliki wa timu hiyo.
Scolari ambaye  kwasasa anaifundisha Brazil yenye wachezaji wengi Chipkizi ameongeza kuwa uamuzi wa kufukuzwa na tajiri wa Chelsea Roman Abromovic  haukuwafurahisha wachezaji wengi kwenye kikosi alichokuwa akikifundisha.
Hatahivyo Scolari amesema kama atapata nafasi ya kurudi England  angependa akaifundishe Chelsea  kwakuwa bado anahitaji kuipa mafanikio mazuri timu hiyo yenye makao makuu yake magharibi mwa jiji la London.

            Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment