Pages

Ads 468x60px

Friday, November 8, 2013

KOCHA WA TIMU YA MBEYA CITY AWASHUKURU MASHABIKI WAO KWA KUWAUNGA MKONO KWENYE DURU YA KWANZA VPL





Baada ya kuiongoza Mbeya City na kumaliza duru ya kwanza ya ligi kuu ya soka Tanzania bara kocha mkuu wa timu  hiyo Juma Mwambusi amewashukuru  wadau na mashabiki kwakuwaunga mkono kwenye michezo yote ya nyumbani na ugenini.
Mwambusi amesema ushirikiano mkubwa walioupata kutoka kwa mashabiki   na wadau umechangia wao kumaliza duru hii bila kufungwa huku wakishika nafasi ya tatu kwenye msimamo nyuma ya Yanga na Azam fc.
Aidha kocha huyo amesema hatarajii kusajili mchezaji nje ya kikosi chao kwenye msimu wa usajili kabala ya  duru ya lalasalama kuanza mwezi  wa kwanza mwakani.
Amesema kama atahitaji kukiongeza nguvu kikosi chake atatumia wachezaji wengine waliyopo kwakuwa anaamini timu hiyo inayoshiriki VPL kwa mara ya kwanza inawachezaji wengi na wazuri.
Pia Mwambusi amesema  mara baada ya mapumziko mafupi timu hiyo itaanzaa maandalizi ya duru ya mwisho kwa kucheza michezo mingi ya kirafiki  kwalengo la kutwaa ubingwa  wa ligi kuu Tanzania bara msimu huu wa 2013/2014.
Katika  duru ya lala salama Mbeya City itaanza  kwakusafiri hadi mkoani Kagera kuifuata Kagera Sukari januari 24  mwakani pambano litakalochezwenye uwanja wa Kaitaba.

Posted by Yusuph Mkule.

No comments:

Post a Comment