Pages

Ads 468x60px

Thursday, November 14, 2013

STEWART HALL ALA SHAVU BAADA YA KUIKACHA AZAM FC.




KOCHA Muingereza, Stewart Hall atakuwa Kocha Mkuu wa akademi ya Symbion Power inayoanzishwa nchini kwa ushirikiano wa klabu ya Sunderland AFC ya England na Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo.
Mtendaji Mkuu wa Symbion Power Tanzania, Peter Gathercole, amesema leo kwamba akademi hiyo itakuwa na vituo Kidongo Chekundu (Sports Park) na Elite Football Academy, Dar es Salaam.


Hall, mwenye leseni ya UEFA ya ukocha na Mkufunzi wa shirikisho hilo, amepewa kazi hiyo baada ya mafanikio yake akiwa na klabu ya Ligi Kuu, Azam FC na timu ya taifa ya Zanzibar na Birmingham City alipokuwa Mkurugenzi wa akademi.  
Kabla ya hapo, Hall alikuwa kocha wa timu za taifa za Saint Vincent na Grenadines, pamoja na Pune FC ya India. 
Akizungumza jana mjini Dar es Salaam, Hall alisema, “Mradi huu hakika utasaidia kuinua soka ya vijana kwa viwango vyote, timu za taifa na klabu. Vijana wadogo watafundishwa ufundi, mbinu, kujengewa uimara wa kimchezo na maarifa ya soka ya kisasa,”alisema.
Mtendaji Mkuu wa Sunderland AFC, Margaret Byrne, amesema: “Tunafurahi mradi wa akademi unaendelea vizuri. Kuteuliwa kwa  Stewart ni hatua ya kufurahisha na tunatarajia kila mmoja kufanya kazi kwa bidii ili kuvuna matunda baadaye.”
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, alitemebelea akademi ya Sunderland akiwa ameambatana na Rais Jakaya Kikwete Juni mwaka huu ambako walifikia makubaliano na Sunderland AFC na Symbion Power Tanzania juu ya mradi huu. 

                                                                           Posted by Yusuph Mkule.


 KIKAO CHA KWANZA JUU YA UKARABATI WA DIMBA LA SOKOINE JIJINI MBEYA  CHAFANYIKA.


Kufuatia uwanja wa Sokine jijini Mbeya kufungiwa kutotumika katika ligi kuu kutokana na kuwa mbovu na timu zinazoutumia kutakiwa kushughulikia ukarabati uongozi wa timu ya Mbeya City umeanza hatua za awali kushughulikia jambo hilo.

Katibu mkuu wa timu hiyo Emanueli Kimbe amesema leo novemba 14  wamekutana na wamiliki wa uwanja huo sambamba na chama cha soka mkoani humo kujadili chakufanya.

Amesema katika kikao hicho kilichohudhuriwa na wawakilishi wa timu ya Tanzania Prisons ya mkoani humo wamejadiliana kwa pamoja na kutoka na kauli ya pamoja kuwa watashirikiana kufanya ukarabati huo.

Hata hivyo ukarabati juu ya dimba hilo unataraji kuanza mara baada ya kufanyika kwa kikao cha wamiliki wa uwanja huo siku ya jumapili na majibu  juu ya ni lini na jinsi gani ukarabati huo utafanyika yatatolewa juma lijalo.

Katika hatua nyingine Kimbe amezionya timu ambazo zinampango wa kuwahadaa wachezaji wao katika msimu huu wa usajili kwa dirisha dogo kuacha mara mmoja harakati zao kwasababu Mbeya City haina mpango wa kuuza mchezaji yeyote.

Pia amesema kama kuna timu inahitaji mchezaji ni vyema ikaonana na uongozi badala ya kuonana na mchezaji wanaomtaka kwakuwa kufanya hivyo ni kosa.

                                           Posted by Yusuph Mkule.

IRFA YATOA UFAFANUZI JUU YA TIMU YA NYANG'ORO KUJITOA KATIKA LIGI YA MKOA WA IRINGA INAYOENDELEA.

 Uongozi wa chama cha mpira mkoa wa Iringa leo umetoa ufafanuzi juu ya kujitoa kwa timu soka ya Nyang’oro iliyokuwa ikishiriki ligi ya mkoa inayoendelea kutimua vumbi mkoani humo.

Katibu mkuu wa chama hicho Eliud Mvela mbali na kutoa ufafanuzi wa timu hiyo kujiondoa amezungumzia suala ya timu mbalimbali ambazo hazijashiriki ligi hiyo msimu huu kwasababu ya kutokuwa na imani na uongozi wa IRFA.

Amesema timu ya Nyang’oro imewasilisha barua ikiomba kujitoa kutoaka na wachezaji wake wengi kujishughulisha na masuala ya kilimo msimu huu hivyo hawawezi kushiriki kikamilifu.

Katika hatua nyingine Mvela  amesema malalamiko yanayotolewa na vilabu ambavyohavijashiriki ligi hiyo msimu huu kutokana na kutofautiana na uongozi wa chama cha mpira sio sahihi.

Amesema ligi inaendeshwa kwa umakini mkubwa na vilabu vinavyokilalamikia chama cha mpira  madai yao hayana ukweli wowote.

Timu za Sengo,Bbc Fc ,Home Boys na Kilolo fc zimejiondoa kushiriki ligi ya mkoa wa Iringa msimu huu kwakulalamikia maamuzi mabaya yanayofanya na waamuzi huku chama cha mpira mkoa kikilalamikiwa kuhusika na timu hizo kuonewa kila msimu wa ligi unapo anza.

                                                  Posted by Yusuph Mkule..

No comments:

Post a Comment