Novemba 23, 2013
TFF
YAUNDA KAMATI NDONGONDOGO
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametangaza wajumbe wa kamati ndogongo (standing committees) wakati zile za haki (judicial organs) na uchaguzi zitaundwa baadaye.
Akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji
kilichofanyika leo (Novemba 23 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, Rais Malinzi
alisema kamati hizo zimeundwa kwa mujibu wa katiba ili kuisaidia Kamati ya
Utendaji.
Pia
ametangaza wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji aliowateua. Wajumbe hao ni
Richard Sinamtwa na Ramadhan Nassib, wakati wengine wanaoingia moja kwa moja
kwenye Kamati ya Utendaji kutokana na kamati wanazoziongoza ni Dk. Paul
Marealle na Saloum Umande Chama.
Kamati
ya Fedha na Mipango inaongozwa na Makamu wa Rais wa TFF, Wallace Karia wakati
wajumbe ni Francis Ndulane (Makamu Mwenyekiti), Omari Walii, Eliud Mvella, Said
Muhammed, Geofrey Nyange, Kidao Wilfred, Ayoub Nyenzi, Lina Kessy na Cyprian
Kuhyava.
Geofrey
Nyange anaongoza Kamati ya Mashindano wakati wajumbe ni Clement Sanga (Makamu
Mwenyekiti), Msafiri Mgoyi, James Mhagama, Mohamed Nassoro, Moses Katabaro,
Seif Ahmed, Gerald ambi, Davis Mosha, Said George na Nassoro Idrissa.
Kinara
wa Kamati ya Ufundi ni Kidao Wilfred wakati wajumbe ni Athumani Kambi (Makamu
Mwenyekiti), Vedstus Lufano, Blassy Kiondo, Rahim Kangezi, Patrick Kahemele,
Daud Yassin, Nicholas Mihayo na Dk. Cyprian Maro.
Kamati
ya Mpira wa Miguu wa Vijana inaongozwa na Ayoub Nyenzi, Khalid Abdallah (Makamu
Mwenyekiti), Ali Mayay, Mulamu Ng’hambi, Apollo Kayungi, Said Tully, Luteni
Kanali Charles Mbuge, Lameck Nyambaya na Ibrahim Masoud.
Lina
Kessy anaongoza Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake wakati wajumbe ni Shyrose
Bhanji (Makamu Mwenyekiti), Zena Chande, Amima Karuma, Dk. Cecilia Makafu,
Zafarani Damoder, Beatrice Mgaya, Sofia Tigalyoma, Martin Mung’ong’o na Engrid
Kimaro.
Kamati
ya Waamuzi inaongozwa na Saloum Umande Chama, Nassoro Said (Makamu Mwenyekiti),
Charles Ndagala (Katibu), Riziki Majala, Kanali Isaro Chacha, Paschal Chiganga,
Victor Mwandike, Soud Abdi na Zahra Mohamed.
Hamad
Yahya Juma ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi anaongoza Kamati ya Habari na
Masoko wakati wajumbe ni Naibu Waziri January Makamba (Makamu Mwenyekiti), Tido
Mhando, Yusuf Manji, Yusuf Bakhresa, Samwel Nyalla, Jack Gotham, Fredrick
Mwakalebela na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania
(TASWA).
Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji inaongozwa na Richard Sinaitwa, Moses Karuwa
(Makamu Mwenyekiti), Zacharia Hanspoppe, Hussein Mwamba, Philemon Ntahilaja,
Abdul Sauko na Imani Madega.
Kiongozi
wa Kamati ya Ukaguzi wa Fedha ni Ramadhan Nassib wakati wajumbe ni Zitto Kabwe
(Makamu Mwenyekiti), Nicholas Magarinza, Jackson Songora, Epaphra Swai, Kalilo
Samson, Goodluck Moshi, Golden Sanga na Elias Mwanjala.
Dk.
Paul Marealle anaongoza Kamati ya Tiba wakati wajumbe ni Dk. Fred Limbanga
(Makamu Mwenyekiti), Dk. Mwanandi Mwankemwa, Dk. Nassoro Matuzya, Dk. Eliezer
Ndelema na Asha Sadick.
RAGE
AAGIZWA KUITISHA MKUTANO SIMBA
Mwenyekiti
wa Simba, Ismail Aden Rage ameagizwa kuitisha Mkutano Mkuu wa Dharura wa klabu
ndani ya siku 14 kuanzia sasa.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa agizo hilo baada ya kubaini kuwa
mgogoro katika klabu baada ya kupokea barua mbili; moja kutoka Kamati ya
Utendaji ikielezea kumsimamisha uongozi Rage, na nyingine kutoka kwa Mwenyekiti
huyo ikielezea kutotambua kusimamishwa huko.
Uamuzi
wa TFF umefanywa kwa kuzingatia Ibara ya 1(6) ya Katiba ya Simba inayosema:
“Simba Sports Club ni mwanachama wa TFF, itaheshimu Katiba, kanuni, maagizo na
uamuzi wa TFF na FIFA, na kuhakikisha kuwa zinaheshimiwa na wanachama wake.”
TFF
itatuma wawakilishi wake katika mkutano huo, na kumuagiza Mwenyekiti wa Simba
kuhakikisha wanachama wote wenye hoja wanapata fursa ya kusikilizwa.
jamali malinzi rais wa shirikisho la soka nchini tff.
Posted by Yusuph Mkule.
Posted by Yusuph Mkule.
No comments:
Post a Comment