Pages

Ads 468x60px

Tuesday, August 12, 2014

TAFADHALI ISOME HII KAMA WEWE NI SHABIKI/MWANACHAMA WA SIMBA UFIKISHE SALAMU KWA UONGOZI WENU.






Waungwana, Mashabiki wapenzi,wanachama wa Simba Sc na wadau Michezo Nchini.. Hizi timu zetu tunazo ziita kubwa hapa nchini sasa zinatakiwa kujitambua, na kulipa fadhira kwa wafuasi wake, badala ya kutuburuza kwa miaka mingi...
Mambo mengi yanaendeshwa kienyeji sana katika Club za Simba na Yanga.. Kiasi mtu unajiuliza hivi izi ndio Club kubwa Nchini Tanzania na E.Africa?
Angalia website ya SimbaSc, ina kua updated kwa mwendo wa kinyonga... Matukio yakipitwa na wakati ndio yanakua breaking news kwenye official website ya timu hii kubwa... Angalia contents za website hii.. Hata vile vitu muhimu tu kwa Website ya Club za soccer hamna.. Hata contact za kuwasiliana na Club hii hamna... Hakuna fixture,hakuna gallery,Kikosi cha timu, team news ndio izo zinachelewa kuakwa..Mapungufu asilimia 75% hadi uvivu kupitia kwenye website ya Club, habar muhimu kuhusu Club una isoma kwa Shigongo kuithibitisha wiki 2 ndio unaipata kwenye Website ya Club...
Me nawapongeza sana Viongozi wa Dar Young Africans kwa kupunguza Matatizo yanayo zuilika kama haya na kilicho baki kwao ni Changamoto tu za hapa na pale.. Website ya Yanga iko active kwa kiasi kikubwa ina contents ANGALAU za kulidhisha kulinganisha na SimbaSc... AzamFc wao ni Another Level sababu wana jua wanacho fanya!
Account zao za Facebook na twitter ziko active na ni reliable kwa habari wanazo toa, ila Account ya SimbaSc ya Twitter ni Majanga vijana wanasema.. Sasa sijui Viongozi husika hawaoni umuhimu wa hizi tools za communication au dharau tu zilizo ota mizizi?.


         Kufukuzwa kwa kocha  Zdravko Logarusic Simba ingetoa maelezo vizuri kupitia website yake nakutoa migongano ambayo ipo miongoni mwa wanachama na mashabiki wao sambamba na kutoa taarifa za ujio wa kocha mpya.                  
                         
                              Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment