Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 14, 2014

SUAREZ APUNGUZIWA ADHABU ILIYOKUWA IKIMKABILI.





                                 Suarez baada ya kung'ata Chiellini.

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Fc Barcelona ya Hispania Luis Suarez amepunguziwa adhabu yake ya kufungiwa miezi minne bila kucheza soka na kutocheza mechi nane kwenye timu yake ya taifa ya Uruguay baada ya rufani yake kusikilizwa leo kwenye mahakama ya kimichezo ya CAS.

Rufani hiyo iliyosikilizwa leo nchini Uswis yalipomakao makuu ya shiriukisho la soka duniani Fifa Suarez sasa ameruhusiwa kufanya mazoezi na klabu yake mpya ya Fc Barcelona lakini adhabu zake zingine zipo palepale.

Suarez mwenye umri wa miaka 27 ambaye aliadhibiwa na Fifa kutokana na kumng’ata nyota wa timu ya taifa ya Italia Giorgio Chiellini kwenye fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil awali alizuliwa hata kufanya mazoezi na wachezaji wa timu yake mpya tangu asajiliwe akitokea Liverpool kwa ada ya uhamisho wa paund milioni 75.

Kupunguzwa kwa adhabu hiyo inamaanisha Suarez atakuwa uwanjani kwa mara ya kwanza akiwa na timu yake ya Barcelona October 26 wakati ambapo itakuwa ikichana na mahasimu wao wakuwa katika ligi kuu ya Hispania Real Madrid.

Aidha tofauti na adhabu yake ya awali amabyo ilimzuia hata kuingia katika uwanja wowote wa soka kwa muda wote wa adhabu hiyo sasa Suarez anaruhusiwa kushiriki masuala mbalimbali yanayohusu soka sambamba na kuhudhuria viwanjani pamoja na kufanya matangazo ya lunigha.

YAFUATAYO NI MATUKIO MHIMU YANAYOMHUSU SUAREZ KATIKA MAISHA YAKE YA SOKA.


June 2014- Aliadhibiwa kutocheza soka kwa miezi minne sambamba na kutoitumikia timu yake ya taifa baada ya kumng’ata mlinzi wa timu ya taifa ya Italia Giorgio Chiellini .
April 2013- Aliomba radhi baada ya kumng’ata mlinzi wa Chelsea raia wa Serbia  Branislav Ivanovic na kisha kuadhibiwa kutocheza mechi 10 za BPL.
Dec 2011- Aliadhibiwa kucheza mechi 8 na faini ya paundi elfu arobaini kwakosa na kumtolea maneno ya kibaguzi aliyekuwa mlinzi wa Manchester United  kwa wakati huo Patrice Evra sasa anakipiga na Juventus ya Italia.
Nov 2010- Aliadhibiwa kutocheza michezo 7 wakati huo akiwa anaichezea Ajax kwa kosa la kumng’ata nyota wa  PSV E indhoven   Otman Bakkal.

HII NI MICHEZO AMBAYO SUAREZ ATAIKOSA YA MSIMU HUU WA LA LIGA KATIKA TIMU YAKE MPYA YA FC BARCELONA.




24 August: Elche (H)
31 August: Villareal (A)
13 September: Athletic Bilbao (H)
16/17 September: Champions League
21 September: Levante (A)
24 September: Malaga (A)
28 September: Granada (H)
30 September / 1 October: Champions League
5 October: Rayo Vallecano (A)
19 October: Eibar (H)
21 / 22 October: Champions League


                      Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment