Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 21, 2014

DZECO ASAINI MKATABA MPYA MANCHESTER CITY.



                                    Edin Dzeco.
Mshabuliaji wa Manchester City Edin Dzeco amesaini mktaba mpya wa miaka minne nasasa ataendelea kusalia Itihadi Stedaum kwa muda mrefu zaidi tangu asajiliwe mwezi wakwanza mwaka 2011 akitokea Wolfsburg ya Ujerumani.

Raia huyo wa Bosnia tangu ajiunge na Mabingwa hao mara mbili  wa ligi lkuu ya  England amefunga magoli 46 kwenye michezo 109 ya ligi kuu na mara baada ya kusaini mkataba huo Dzeco amesema anajisikia fuha kuendelea kubaki City.

Dzeco ambaye msimu wa 2012/2013  alifunga magoli 15 kwenye michezo 44 nakuibuka mfungaji bora wa timu hiyo amesema City  anafarijika kuichezea timu hiyo na kufurahia mafanikio yanayopatikana klabuni hapo.

Dzeco ambaye ni miongoni mwa wachezaji wa Bosnia walioshiriki fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil kabla ya kusajiliwa na Manchester City akiwa Wolfsburg aliweka historia ya kufunga magoli 66 kwenye michezo 111 ya Bundesliga.


                        Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment