Pages

Ads 468x60px

Tuesday, August 12, 2014

MO FARAH ATOBOA SIRI YA KUTOSHIRIKI MICHUANO YA JUMUIA YA MADOLA MWAKA HUU.



Mwanariadha wa uingereza Mo Farah ameweka hadharani sababu zilizomfanya ashindwe kushiriki mashindano ya jumuia ya Madola yaliyomazika hivi karibuni mjini Glascow Scotland kwakusema matatizo ya moyo ndiyo chanzo kikuu.
Farah mwenye umri wa miaka 31 amesema tatizo hilo liligundulika alipoanguka bafuni baada ya kutoka kwenye mazoezi mwanzoni mwa mwezi wa tatu mwaka huu na kilichomsaidia ni simu aliyokuwa nayo ambayo aliitumia kumwita mwenzake amsaidie.

Baada ya hapo Farah amesema alikimbizwa hospitali na kukaa siku nne  akitibiwa kabla ya kuruhusiwa  na kusisitiza kuwa kwa muda wote huo alikuwa akihisi  maumivu makali tumboni.
Mshindi huyo wa mbio za mita elfu tano na mita elfu kumi  katika mashindano ya Olympic amesema mara baada ya uchunguzi kufanyika iligundulika kuwa  kuna kasoro katika mapigo yake ya Moyo.

Farah ambaye kwasasa amepona na amewaomba radhi mashabiki wake wengi waliokuwa wamekata tiketi kushudia michezo ya jumuia ya madola  huku akisema kuwa hakutazama mchezo hata mmoja kwenye michuano ya jumuia ya madola.


Kwasasa Farah anajiandaa kushiriki michuano ya European Championships mjini Zurich Uswis ambayo inaanza leo tarehe 12 hadi 17 ya mwezi huu wa nane na anamatumaini makubwa yakurejea uwanjani katika kufukuza upepo.
                         Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment