Pages

Ads 468x60px

Sunday, August 10, 2014

MATS HUMMELS NAHODHA MPYA WA BORUSSIA DORTMUND.








Klabu ya Borussia Dortmund uya Ujerumani imemteua mlinzi wa kati wa timu hiyo Mats Hummels kuwa nadhodha wa mpya   atakekuwa akisaidiwa na Marco Reus pamoja na Roman Weidenfeller.
Hummels mwenye umri wa miaka 25 ameteuliwa na kocha mkuu wa kikosi hicho Jurgen Klopp licha ya nyota huyo kuhusishwa na kuhamia Manchester United kwa siku kadhaa sasa.
Taarifa zimesema kuwa uamuzi wa mlinzi huyo kupewa jukumu la unahodha linatokana na Sebastian Kehl  ambaye alikuwa nahodha  kutangaza kutovaa tena kitambaa hicho kutokana na kutocheza  mara kwa mara.
Hummels ambaye leo ameshuhudia timu yake ikufungwa magoli 4 kwa 0 na Liverpool kwenye mchezo wa kirafiki amepewa jukumu hilo la unahodha siku tatu kabla ya timu yake kukutana na Bayern Munich kwenye mchezo wa German Supercup.

                    Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment