Pages

Ads 468x60px

Thursday, August 7, 2014

NEYMAR YUPO FITI ,SASA KUCHEZA MCHEZO WA KWANZA WA LA LIGA.




Picha ndogo kwa juu ikionyesha jeraha alilolipata katika fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.

Baada ya kupatiwa matibabu mshambuliaji wa Fc Barcelona na timu ya taifa ya Brazil Neymar  anaweza kuwa fiti tayari kwa msimu mpya wa La Liga  kufuatia kufaulu vipimo jana jumatano.

Awali nyota huyo aliyeumia mwishoni mwa mashindano ya kombe la dunia nchini Brazil mwaka huu ilikuwa inatajwa huenda atakaa muda mrefu nje ya uwanja baada ya kuumia uti wa mgongo.
Taarifa  kutoka katika klabu ya Fc Barcelona imesema nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 amefaulu vipimo alivyofanyiwa na madaktari wa timu hiyo hivyo upo uwezekano akacheza mchezo wa ufunguzi katika ligi ya Hispania dhidi ya Elche.
Klabu ya Fc Barcelona  jana jumatano imethibitisha kuwa Neymar na wachezaji wengine watatu walioshiriki fainali za kombe la dunia mwaka huu wamefaulu vipimo maalumu na sasa wapotayari kwa mazoezi ya msimu mpya.

                      Neymar akiwa chini baada ya kuumizwa na Zuniga.

Awali Neymar alikuwa anakadiriwa kukaa nji ya dimba kwa wiki sita hali iliyokuwa inatishia Barcelona kumkosa  kwenye mechi ya ufunguzi wa La liga dhidi ya Elche Augost 23 kutokana na jeraha la mgongo alilolipata kwenye pambano baina ya timu yake ya Brazil na Colombia ambapo mlinzi wa Colombia Juan Camilo Zuniga alimchezea rafu mbaya.
Mapema wiki hii Barcelona imethibitisha wachezaji wake wanne waliokuwepo na timu zao za taifa kwenye fainali za kombe la dunia zilizofanyika mwaka huu nchini Brazil wamewasili na wamefaulu vipimo walivyofanyiwa  ili kuhakiki Afya zao kabla ya kuanza kwa ligi.
Wachezaji hao ni Leo Messi, Javier Mascherano, Dani Alves  na Neymar na wote kwa pamoja watakuwa kwenye mazoezi ya wiki tatu klabya ya ligi kuanza.
Mlinzi Adriano  ambaye anasumbuliwa na tatizo la kuwa na mapigo ya moyo yasiyo yakawaida bado anaendelea na matibabu wakati kiungo Xavi na nyota mpya wa timu hiyo  Jeremy Mathieu wao watakuwa wakifanya mazoezi ya tofauti na kikosi.

                       Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment