Pages

Ads 468x60px

Sunday, August 24, 2014

SMAILLING KULAMBA MKATABA MPYA MANCHESTER UNITED.



                                         Chris Smalling.
Klabu ya Manchester United ya Uingereza inajiandaa kufanya mazungumzo na mlinzi wale Chris Smailling  kwaajili ya kumpatia mkataba mpya wa miaka mitano majuma machache yajayo.
Mashetani hao wekundu wa Old Traford wamepanga kumwongeza mshahara mchezaji huyo  hadi kufikia paundi elfu sabini kwa wiki  kama njia ya kumshawishi kubakia klabuni hapo baada ya Arsenal kuanza kumnyemelea.
Mlinzi huyo wa nafasi ya katikati na pembeni kwasasa analipwa mshahara wa Euro elfu sitini na mbili  utakaomfanya awe sawa na muingereza mwenzake Phil Jones ambaye wote wanaichezea timu hiyo ya Manchester United.
 
Wakat huohuo Manchester United  imekaribia kumsajili Angel Di Maria kutoka Real Madrid kwa uhamisho  wa kati ya Euro milioni 60 hadi 70  baada ya mchezaji huyo kugoma kuongeza mkataba mpya na tayari ameandika waraka kwa mashabiki wa Real  akieleza sababu za kuhama Santiago Bernabeu.
                                       Angel di Maria.

                           Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment