Pages

Ads 468x60px

Sunday, August 3, 2014

LAMPARD KUANZA MAZOEZI JUMATANO IJAYO NDANI YA MANCHESTER CITY.




                                            Frank Lampard.

Kocha mkuu wa timu ya Manchester City Manuel Pellegrin amethibitisha kuwa kiungo Frank Lampard anataraji kuanza mazoezi na kikosi chake baada ya kujiunga na mabingwa hao wa ligi kuu ya England kwa mkopo akitokea New York City ya Marekan.

Pellegrin ambae ni raia wa Chile amesema kiungo huyo aliyesajiliwa na New York City akitokea Chelsea atalazimika kupigania namba kwenye kikosi chake hadi hapo atakaporejea katika ligi kuu ya Marekani  MLS mwezi wa kwanza mwakani.

Kocha huyo amesema Lampard anataraji kuanza mazoezi na Manchester City jumatano ya wiki ijayo na atakuwa katika kikosi hicho na kucheza michezo mbalimbali itakayokuwepo kwenye ratiba yao msimu wa 2014/2015.

Pamoja na uvumi kuwepo kwamba Lampard husnda asijeze michezo ambayo City itakuwa ikiikabili Chelsea kocha Manuel Pellegrin amesema hakuna jambo kama hilo kiungo huyo aliyesajiliwa kwa mkopo wa miezi 6 atacheza kama wachezaji wengine.
                                     Frank Lampard ndani ya uzi wa New York City.

                               Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment