Pages

Ads 468x60px

Sunday, August 3, 2014

VAN PERSIE KUKOSA MICHEZO YA MWANZO YA MSIMU WA LIGI 2014/2015.




                                                                Robin van Persie.

Timu ya Manchester United ya England inataraji kumkosa mshambuliaji wake  Robin van Persie mwanzoni mwa msimu mpya wa ligi  ambaye amerefushiwa muda wa mapumziko baada ya kuwepo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi. 

Kocha mkuu wa Manchester United Louis van Gaal amesema mchezaji huyo ambaye bado yupo mapzikoni anataraji kuanza mazoezi kesho jumatatu hivyo atatakiwa kuwa na muda mrefu wa kujifua zaidi.

Van Gaal ambaye alikuwa na kikosi cha timu ya taifa Uholanzi kilichoshika nafasi ya tatu kwenye kombe la dunia zilizomalizika mwezi uliopita nchini Brazil amesema Van Persie hatocheza mchezo wowote wa kujiandaa na msimu mpya utakaoanza katikakati ya mwezi huu.

United ambayo inataraji kukata utepe wa ligi kuu ya England na Swansea City tarehe 16 ya mwezi huu kwenye uwanja wake wa Old Traford  imeendelea kufanya vyema katika michezo yake ya majaribio nchini Marekani baada ya jana kuifunga Real Madrid magoli 3 kwa1.
  

               Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment