Pages

Ads 468x60px

Saturday, August 2, 2014

RONALDO KUUKOSA MCHEZO BAINA YA REAL MADRID NA TIMU YAKE YA ZAMANI MANCHESTER UNITED LEO.




                                                           Cristiano Ronaldo.

Wakati Real Madrid ikijiandaa kuikabili Manchester United leo katika pambano la kirafiki mjini Michingan nchini Marekani mshambuliaji Cristiano Ronaldo ataukosa mchezo huo na badala yake atakuwepo kwenye pambano la European Super Cup.

Kocha mkuu wa Real Madrid Carlo Ancelotti amesema mchezaji huyo anaendelea na mazoezi binafsi  kutokana na maumivu ya goti yanayomsumbua lakini anataraji kujumuika katika mazoezi ya pamoja na wenzake Augost 5 mwaka huu.

Ancelottamesema Ronaldo anataraji kucheza mchezo wa European Super Cup dhidi ya Real Sosiedad  na kwenye pambano dhidi ya mabingwa wa Europa League Sevilla mjini Cardif Augost 12 mwaka huu.

Mchezo wa kirafiki leo dhidi ya Manchester United ni wa kuhitimisha ziara ya Real Madrid nchini Marekan na kocha mkuu wa timu hiyo Carlo Ancelotti amesema wanajivunia kuwa na maandalizi mazuri ya msimu mpya wa ligi nchini humo.

Real Madrid ambayo itafungua pazia la ligi kuu ya Hispani dhidi ya Cordoba Augost 25 mwaka huu  mchezo wao wa kwanza wa Spanish Super Cup dhidi ya Atletico MADRID UTACHEZWA Augost 19  Santiago Bernabeu na ule wa marejeano utachezwa Augost 22 mjini Calderon.


                    Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment