Pages

Ads 468x60px

Friday, August 1, 2014

RASMI MAGURI ATUA SIMBA AMWAGA WINO WA KUVAA UZI MWEKUNDU KWA MIAKA 2.







                                        Kifaa kipya cha Simba -Eliass Maguri.

Hatimae klabu ya Simba ya jijini Daresalaam leo imekamilisha usajili wa aliyekuwa mshambuliaji wa maafande wa Ruvu Shooting kutoka mkoani Pwani Elias Maguri.

Maguri ambaye sakata lake la kwenda Simba lilitawala katika vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini takribani majuma mawili amesaini mkataba wa miaka miwili kukipiga na wekundu hao wa msimbazi Simba.

Dili ya Maguri kutua msimbazi limekamilika leo mbele ya makamu wa rasi wa klabu hiyo ya Simba  Geoffrey Nyange ‘Kaburu amesema wanaimani kubwa na mchezaji huyo kwamba atawasaidia katika miaka yake miwili atakayokuwa Simba.
                   Eliass Maguri mwenye jezi ya kijani akiwa mzigoni.

Mbali na kuichezea Ruvu Shooting ya Pwani Maguri pia amewahi kukipiga na maafande wa Tanzania Prisons wenye maskani yao jijini Mbeya.

Kusajiliwa kwa Maguri ni mwendelezo wa vita ya usajili hapa nchini ambayo itaendelea hadi katikati ya mwezi huu wa nane mwaka 2014.

                             Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment