Ruud van Nistelrooy.
Shirikisho la soka nchini Uholanzi (KNVB) limemteua mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Manchester United na Real Madrid Ruud van Nistelrooy kuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa hilo
Nestelorooy ambaye alifunga magoli 35 kwenye michezo 70 aliyocheza katika timu ya taifa ya Uholanzi enzi za uchezaji wake atakuwa akifanya kazi chini ya kocha mkuu mpya wa taifa hilo Guus Hiddink sambamba na Danny Blind.
Shirikisho hilo la soka la Uholanzi pia limemteua Patrick Lodewijks kuwa kocha wa makipa akichukua nafasi ya Frans Hoek aliyeungana na Louis van Gaal kwenda Manchester United huku Patrick Kluivert akienguliwa katika benchi la ufundi la timu ya Uholanzi.
Katika hatua nyingine shirikisho
hilo limewateua Pierre van Hooijdonk, Aron Winter, Sonny Silooy na
Michael Reiziger kuwa wasimamizi wa timu za taifa za vijana za nchi hiyo.
Mkule.blogsport.com
No comments:
Post a Comment