Pages

Ads 468x60px

Friday, August 1, 2014

MOURINHO AFUNGUA MLANGO WA KUTOKEA KWA CECH.






Kocha mkuu wa Chelsea Jose Mourinho ametangaza kuwa mlindamlango namba moja wa timu hiyo Petr Cech huenda akaihama klabu hiyo msimu huu.

Kauli ya Mourinho imekuja kukiwa na tetesi kuwa  huenda  mlinda mlango wao aliyekuwa kwa mkopo katika timu ya Altetico Madrid Thibaut Courtois akarejea kwa matajiri hao wa jijini London.

Imeelezwa kuwa Chelsea ipotayari kusikiliza ofa kutoka PSG iliyoonyesha nia ya kutaka kumsajili Cech  huku Morinho akijiandaa kumfanya Mark Schwarzer kuwa mlinda mlango namba mbili baada ya kuja kwa Thibaut Courtois.

Pamoja na Mourinho kukiri Cech yupo tayari kupigania namba kwenye kikosi chake cha Chelsea amesema Thibaut ni mlinda mlango mzuri na chipkizi anayefanya vyema kwenye ulimwengu wa sasa na hilo halina ubishi wowote.

Kwaupande wake Thibaut ameiambia tovuti ya Chelsea kuwa anajisikia furaha kuwa mchezaji wa timu hiyo na anajisikia faraja kubwa kwa mapokezi mazuri aliyoyapata kwenye timu hiyo ya jijini London.

                                                               Thibaut Courtois.


                              Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment