Shirikisho la soka barani
Ulaya Uefa limethibitisha kuwa litanza uchunguzi juu ya vurugu zilizojitokeza katika mchezo wa hatua
ya makundi msimu uliopita baina ya timu ya Dnipro na Fc Copenhagen ambao
ulichezewa kuanza kwa dakika 10.
Taarifa ya Uefa imesema
uchunguzi huo utalenga sababu za mashabiki kuvamia uwanja mjini Ukrain na
kufanya timu hizo kurudi katika vyumba vya kubadilishia nguo kabla ulinzi
kuimarisha na pambano hilo kuendelea.
Wakati Uefa ikithibitisha kufanyika kwa uchunguzi huo mkurugenzi mkuu wa timu ya FC Copenhagen Anders Horsholt amesema ghasia hizo za mashabiki zilitokana na tatizo la ulinzi kwenye uwanja wa timu ya Dnipro.

Katika ghasia zilizojitokeza
kwenye mchezo huo takribani mashabiki 30 wa Fc Copenhagen walikamatwa na askari
wakiwa na bendera pamoja na mabango mbalimbali taarifa hiyo imeeleza.
Mkule.blogsport.com
No comments:
Post a Comment