Pages

Ads 468x60px

Friday, August 1, 2014

DZEKO AONGEZA MKATABA SASA KUBAKIA MANCHESTER CITY HADI 2018.




                                                                        Edin Dzeko.
Mabingwa wa ligi kuu ya England Manchester City wamefikia makubaliano ya kumwongeza mkataba wa miaka mine na mshambuliaji Edin Dzeco utakaomfanya aitumikie timu hiyo hadi mwaka 2018.

Dzeco ambaye alikuwa amebakisha mwaka mmoja  kwenye  mkataba wake wa zamani pamojana na kuongezwa mkataba ataendelea kulipwa mshahara wake ule ule aliokuwa akilipwa wa Euro laki moja na themanini na tisa elfu kwa wiki.

Mshambuliaji huyo ambaye alikiwa kwenye mipango ya kuihama timu hiyo wakati ikiwa chini ya kocha  Roberto Mancin kabla ya kuja kwa kocha mpya Manuel Pellegrini msimu uliopita alifanikiwa kufunga magoli 26 katika michezo 23.

Dzeco amekuwa mchezaji wa tatu kupewa mkataba mpya na timu hiyo msimu huu akiungana na Alexsandar Kolarov na Samir Nasri ambao wamesaini mikataba mipya mwezi wa sita na wa saba mwaka huu.
                       
                        Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment