Pages

Ads 468x60px

Monday, August 4, 2014

NASRI KUTANGAZA HATIMA YAKE YA KUCHEZEA TIMU YA TAIFA.




Samir Nasri.


 Kiungo wa klabu ya Manchester City ya England Samir Nasri amesema anataraji kutangaza hatima yake ya kuichezea timu ya taifa ya Ufaransa au kutoichezea tena katika maisha yake ya soka siku chache zijazo.

Nasri ambaye aliachwa kwenye kikosi cha Ufaransa kilichoshiriki fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil amesema tayari ameshafanya maamuzi yake na anataraji kuyatangaza rasmi.

Kiungo huyo ambaye vitendo vya utovu wa nidhamu ndivyo vilivyomfanya aachwe na kocha mkuu wa Ufaransa Didier Deschamps ameeleza kuwa suala la kucheza au kutohitaji kucheza kwenye timu ya taifa atalitangaza katika mahojiano maalumu.

Nasri amesema hajashinda taji lolote na timu ya taifa jambo ambalo halimpi ugumu wa kutangaza kutoendelea kuichezea timu yake ya taifa tofauti na kama angekuwa ameshinda mataji mengi lingekuwa jambo gumu kwake.

                          Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment