Pages

Ads 468x60px

Monday, August 4, 2014

RORY MCILROY AMEJEA KATIKA NAFASI YA KWANZA KWA UBORA WA GOLF DUNIANI.



                                   Rory McIlroy akipokea taji la WGC.
 
Mcheza Golf Rory McIlroy amejea katika nafasi ya kwanza kwa ubora wa mchezo huo duniani baada ya kufanikiwa kushinda taji la WGC-Bridgestone mjini Ohio akimshinda Sergio Garcia.
 
McIlroy  ameshinda taji hilo la WGC kwa mara ya kwanza  nakumfanya amwengue  raia wa Australia Adam Scott kwenye nafasi kwanza ambayo alikalia tangu mwezi wa tatu mwaka jana.

Akizungumzia ushindi alioupata Mcllroy amesema anajivunia kupata mafanikio hayo huku akisifu uwezo mkubwa aliouonyesha  nakuahidi kuwa atahakikisha analinda kiwango chake kidumu msimu huu wote.

Katika hatua nyingine  mcheza Golf Tiger Woods  yupo kwenye hatari ya kushiriki mashindano ya  PGA nchini Marekani na Ryder Cup mwaka huu  kutokana na kusumbuliwa na  maumivu ya mgongo.

                                  Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment