Pages

Ads 468x60px

Wednesday, July 16, 2014

WAJUKUU WA MANDELA WAWASILI KUWAVAA SERENGETI BOYS.





                   Kikosi cha U-17 cha Afrika ya kusini.

Kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 cha Afrika Kusini (Amajimbos) kimewasili nchini kuikabili Tanzania (Serengeti Boys) katika mchezo wa kwanza wa raundi ya pili wa michuano ya Afrika utakaochezwa keshokutwa (Julai 18 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.

Kikosi cha Amajombos chenye msafara wa watu 37 kilitua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jana usiku  na kimefikia hoteli ya Sapphire nah ii leo kilitarajiwa kufanya kwenye Uwanja wa Azam Complex.



          Kikosi cha timu ya vijana ya Afrika ya Kusini U-17.

Waamuzi watakaochezesha mchezo huo Shelisheli wakiongozwa na Allister Barra tayari wamewasili nchini sambamba na kamishna wa mchezo huo Andriamiasasoa Doda Nirimboavonjy kutoka Madagascar.

 Kikosi cha Serengeti Boys chini ya kocha Hababuu Ali Omari kipo kambini kwa zaidi ya majuma mawili sasa kikijiandaa kwa mchezo huo.

                           Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment