Pages

Ads 468x60px

Tuesday, July 22, 2014

MAN CITY YAPATA PIGO NEGREDO AUMIA.




Mshambuliaji wa timu ya Manchester City,Alvaro Negredo anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa miezi kadhaa kutokana na kuumia mguu wa kulia kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya hearts.
Negredo mwenye umri wa miaka 28 amethibitisha taarifa hizo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram akiambatanisha pamoja na picha ya mguu huo wenye majeraha.
Nyota huyo amewataka mashabiki  wa Manchester City kutokuwa na hofu juu yake katika kipindi hiki kigumu ambacho atakuwa nje ya uwanja kwa mda mrefu.
Taarifa hizo zitakuwa ni mbaya kwa Kocha wa kikosi hicho, Manuel pellegrin wakati wakijiandaa kutetea ubingwa wao wa ligi kuu England kwa msimu unao kuja.

                       Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment