Pages

Ads 468x60px

Sunday, July 27, 2014

ANCELOT:BADO NINA MIPANGO NA DI MARIA.




 
                                                  Angel Di Maria.

Licha ya kuwepo kwa taarifa  mbalimbali zinazomhusisha nyota wa Real Madrid Angel Di Maria kuihama timu hiyo kocha Carlo Ancelotti amesema mchezaji huyo bado yupo kwenye mipango yake msimu ujao.

Ancelotti amesema Di Maria mwenye umri wa miaka 26  bado ni mchezaji wa Real Madrid  na klabu hiyo itaendelea vizuri na masuala yake ya uhamiso hadi siku yake ya mwisho akiwa Santiago Bernabeu.

Kocha huyo raia wa Italia amesema baada ya ujio wa wachezaji wawili wapya msimu huu wa usajili kikosi chake kimeimarika na kuwa cha ushindani kuliko msimu uliopita.

Di Maria ambaye alijiunga na Real Madrid mwaka 2010 akitokea Benifica ya Ureno amekuwa akihusishwa na mipango ya kuhamia PSG ya Ufaransa na pia Manchester United ya Uingereza nayo imekuwa ikitajwa kumwania mchezaji huyo raia wa Argentina.

                                Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment