Fabio Borini akiwa na ndani ya uzi wa Liverpool.
Timu ya Liverpool imefikia makubaliano ya kummuza
mshambuliaji Fabio Borini kwenda
Sunderland kwa uhamisho fa paundi milioni 14.
Borini mwenye mwenye umri wa miaka 23 alikuwa Sunderland kwa mkopo msimu uliopita na kuisaidia timu hiyo kukwepa janga la
kushuka daraja.
Katika msimu uliopita raia huyo wa Italia alikwamisha kimiani
magoli 10 na kunyakua tuzo ya mchezaji bora chipkizi wa timu hiyo kwa msimu
huo.
Licha ya nyota huyo kupigania namba kwenye kikosi cha Liverpool
na kufunga magoli 2 msimu wa 2012/2013 haikutosha kumshawishi kocha Brendan
Rodgers jambo liliofanya atolewe kwa mkopo kwenda Sunderland.
Borini alikuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha Brendan
Rodgers kutoa Roma ya Italia kwa dau la paundi milioni 11 mwezi july mwaka
2012.
Mbali na kuinusuru Sunderland isishuke daraja msimu uliopita
Borini aliiwezesha Sunderland kufikia hatua ya fainali kwenye kombe la Capital
one licha ya kikosi hicho kufungwa na Manchester City kwenye fainali.
Kama atajiunga na Sunderland mmoja kwa mmoja Borini atakuwa
mchezaji wa 4 kusajiliwa msimu huu baada ya kiungo Jordi Gomez kutoka
Wigan,mlinzi Billy Jones kutoka West Brom na mlindamlango Costel Pantilimon
kutoaka Manchester City.
Mkule.blogsport.com
Liverpool wamepoteza jembe.
ReplyDeleteKweli kama aliisaidia Sunderland isishuke daraja huyo alikuwa mtu mhimu sana kusalia Liverpool.
ReplyDeleteAcha aende zaje tutapata jembe ligine kali zaidi yake.
ReplyDelete