Pages

Ads 468x60px

Friday, July 18, 2014

ARTURO VIDAL AKIRI YUPO NJIAPANDA KWASASA.MAN UNITED MPO?





                                        Arturo Vidal

 Maombi ya mashabiki wa Manchester Unite kuwa na nyota wa Juventus Arturo Viadl msimu ujao huenda yakawa yanakaribiwa kujibiwa na mungu baada ya mchezaji huyo raia wa Chile kuweka wazi kwamba hadhani kama atakuwepo Italia msimu ujao.

Kiungo huyo ambaye amekuwa akifukuziwa kwa karibu na Manchester United amekaririwa na gazeti moja la nchibni Chile lijulikanalo kama  La Cuarta akisema  ni vigumu kuzungumzia timu kubwa ukiwa ndani ya klabu yenye mafanikio kama Juve ambayo ameshinda mataji  3 ya ligi kuu ya Italia.

kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 amesema anaziheshimu timu ambazo zimeonesha nia ya kutaka kumsajili Real Madrid na Manchester United lakini juu ya maombi yao anayeweza kuvizungumzia ni wakala wake ambaye ndiye msimamizi wake.

Nyota huyo ambaye alisajiliwa na Juventus mwaka 2011 kwa Euro milioni 10.5 kutoka Bayer Leverkusen amesema hadi sasa hajui kama atabakia katika timu yake na mara baada ya kurejea Italia akitokea kwao Chile ataonana na kocha mpya Massimiliano Allegri kuona kipi kitafuata.

Hii ni kauli yake aliyoitoa…"I honestly do not know if my cycle with Juventus is finished. When I return to Italy I will talk with the new coach and see what happens.

                             Mkule.blogsport.com

No comments:

Post a Comment