Mo Farah.
Mwanariadha Mo Farah amejitoa kushiriki mashindano ya Commonwealth mjini Glasgow nchini Scottland baada ya kuchelewa kupona haraka homa.
Frah mwenye umri wa miaka 31 amewahi kushinda mbio za mita elfu tano na mita elfu kumi mjini Londoni mwaka 2012 na alikuwa ashiriki mbio hizo katika michuano hiyo ya mwaka huu nchini Scotland.
Mwanariadha huyo licha ya kuamua kubaki katika kambi ya ya mazoezi kujiweka fiti kwaajili ya mashindano ya European Championships mjini Zurich Uswiss amesema amejisikia vibaya kutoshiriki mashindano ya Commonwealth mwaka huu.
Wafuatao ni wanariadha ambao hawatakuwepo kwenye mashindano ya Commonwealth mwaka huu mjini Glasgow.
Yohan Blake (Jamaica) - Ex-world 100m champion- hamstring operation |
Mark Cavendish (Isle of Man) - Ex-world champion cyclist - shoulder injury |
Dwain Chambers (England) - British 100m champion - Euro focus |
Jessica Ennis-Hill (England) - Olympic heptathlon champion - had a baby |
Mo Farah (England) - Olympic 5,000m & 10,000m champion - illness |
Becky James (Wales) - Two-time world champion cyclist - knee injury |
Katarina Johnson-Thompson (England) - Heptathlon star - foot injury |
Asafa Powell (Jamaica) - Ex-world 100m record holder - banned |
Mjamaika Yohan Blake ambaye ni mshindi wa medali ya fedha kwenye mbio za 100 na 200 katika michuano ya Olympic mwaka 2012 mjini London ameshindwa kushiriki michuano hii ya Commonwealth kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya misuli ya paja huku Muingereza Karatina Johnson-Thomptos akijitoa kutokana na kuumia mguu.
Mkule.blogsport.com
No comments:
Post a Comment